Njia bora ya kupokea bidhaa uagizapo mtandaoni

Mara nyingi watu wengi hujiuliza ni kwa njia gani naweza kupokea mzigo wangu niagizapo mtandaoni?
kwa hapa Tanzania njia rahisi kabisa kupokea mzigo wako yenye gharama nafuu ni kwa
kutumia anuani ya sanduku la posta.
Sio lazima uwe na sanduku la posta, unaweza andika hata sanduku la posta la rafiki au ndugu yako la mkoa ambao unahitaji kupokelea mzigo wako kutoka nchi za nje.
Posta wana utaratibu wa kutuma ujumbe wa simu kwa wateja wao waliotumiwa mizigo kutoka nchi za nje, hivyo basi kwenye anuani hakikisha  unaandika namba  ya simu iliyo sahihi ili mzigo wako ukifika uweze kutumiwa ujumbe kutoka posta ili ukauchukue.
ukiona hujapata ujumbe, tembelea sanduku la posta ulilotumia kama anuani ya kupokelea mzigo, fungua na angalia kama kuna karatasi zenye taarifa ya mzigo wako.
ukiona zipo zichukue kisha nenda nazo ndani ya ofisi waonyeshe karatasi wahusika waambie umekuja kuchukua mzigo wako.
je, kuna gharama yoyote ya kulipia?
kama mzigo ukifika Tanzania na namba ya kupokelea mzigo iliyoandikwa kwenye karatasi ikianza na     neno FGN ikifatiwa na namba kadhaa ujue hapo huto lipia gharama yoyote ile. mfano FGN-18-226163.
lakini kama namba ya mzigo kwenye karatasi au message uliyotumiwa ikianza na neno DP au RDP ikifuatiwa na namba kadhaa mfano DP-18-2213 hapo ujue unatakiwa kulipia pesa kidogo ambayo ni TSHS. 1500 tu.
Kuhusu kodi inakuaje?
mzigo wenye namba zinazoanza na DP au FGN haulipiwi kodi yoyote ile lakini mzigo unaonza na neno RDP unalipiwa kodi hapo hapo ofisi za posta.
endelea kusoma masomo yetu upate uelewa zaidi na usiogope tena kununua bidhaa mtandaoni.

Featured Post

Jifunze kununua mtandaoni

Karibu katika somo la kwanza ujifunze ni jinsi  gani unaweza kununua bidhaa kutoka mataifa makubwa duniani kwa kutumia mitandao mikubwa ka...