1. Hakikisha kadi yako imewezeshwa kufanya malipo kutoka benki husika
2. Angalia kama umepewa ticket za zawadi.
Hatua ya kwanza na ya muhimu ni kujua kama kadi (mastercard) yako imezeshwa kufanya malipo mtandaoni.
Kutokana na changamoto za kiuelewa na kiufahamu bank nyingi za Tanzania kama CRDB na NMB huwa hazirusu manunuzi ya mtandaoni moja kwa moja. Jambo la kufanya ni kutumbelea tawi husika na kujaza form ambayo itaruhusu kadi yako kuwezeshwa kufanya malipo mtandaoni na baada ya hapo hatua nyingine zinaweza kufuata kiurahisi.
Kutokana na changamoto za kiuelewa na kiufahamu bank nyingi za Tanzania kama CRDB na NMB huwa hazirusu manunuzi ya mtandaoni moja kwa moja. Jambo la kufanya ni kutumbelea tawi husika na kujaza form ambayo itaruhusu kadi yako kuwezeshwa kufanya malipo mtandaoni na baada ya hapo hatua nyingine zinaweza kufuata kiurahisi.
Baadhi ya wauzaji wa mtandaoni mfano amazon.com hutoa kuponi za zawadi kwa ajili ya wanunuzi wapya ambazo hutumwa kwa njia email. Hivyo basi unapofanya manunuzi mara kwa mara au manunuzi makubwa ni muhimu kuangalia kama umepata kuponi ya punguzo ambayo itakuwezesha kununua bidhaa kwa bei nafuu zaidi. Baadhi ya watu hupuuzia kuponi hizo na kukosa unafuu katika manunuzi yao.
3. Chagua njia sahihi ya kusafirisha mzigo wako
Kati ya mambo ya msingi ya kufahamu unapotaka kuweka oda ya mzigo wako ni aina ya usafiri ambayo utaitumia hili ni jambo la muhimu kutokana na ukweli kwamba bidhaa hutofautiana katika urahisi wa kuvunjika au kuharibika. Vile vile suala la bidhaa kufika ndani ya muda huwa ni la muhimu pia. Unapoagiza bidhaa mtandaoni kuna plan tofauti za usafirishaji kuanzia free shipping, moderate plan, fast plan, standard plans (kutegemeana na e-commerce). Jambo la kuzingatia hapa ni kuangalia namna mzigo wako utakavyokufikia, baadhi ya njia huwa na changamoto za ufikishwaji wa mizigo, kwa mfano njia ya meli huchelewa ukilinganisha na njia ya ndege.
4. Hakikisha maelezo ya bidhaa unayoagiza kwa usahihi
Ni muhimu kusoma maelezo yote ya bidhaa hususani bidhaa zenye gharama kubwa na za kielectronics baadhi ya wanunuzi hupuuzia kusoma maelezo ya bidhaa na kusababisha kuagizwa kwa bidhaa iliyo na vigezo vingine, tofauti na kile walichokuwa wakikitarajia. Katika kila bidhaa inayowekwa mtandaoni huwa na kipengele cha maelezo ya ziada (products description) hivyo basi ni jambo la msingi kwa mnunuzi kusoma maelezo yote kabla ya kufanya malipo.
5. Angalia mrejesho wa wanunuzi wengine
Jambo jingine la msingi ni kuangalia maoni ya wanunuzi wengine au ratings. Mifumo mingi ya e-commerce inatoa nafasi kwa wanunuzi wengine kuweka maoni ya bidhaa, baada ya manunuzi. Ni jambo la msingi kwa mnunuzi kupitia maoni ya wateja wengine walionunua bidhaa za aina hiyo ili kujiridhisha na ubora wa kitu anachotaka kukinunua mtandaoni. Endapo wateja wengine watakuwa na malalamiko ya bidhaa ni vema mnunuzi ukatafuta muuzaji mwngine mwenyee maoni mazuri.
6. Fahamu gharama za kodi za kitu unachokinunua
Kilanchi huwa na gharama tofauti za kodi. Jambo la msingi kwa mnunuzi ni kujua gharama za kodi za nchi yake. Sio bidhaa zote zinazotakiwa kulipiwa kodi, hivyo ni suala la elimu sahihi kwa mnunuaji pale anapopokea mzigo. Jambo la msingi katika kipengele cha kodi ni mawasiliano mazuri baina ya muuzaji na mnunuaji ili kufanya marekibisho ya bei inayoandikwa wakati wa kuagizwa kwa mzigo.
7. Tunza kumbukumbu zote zinazohusiana na mzigo wako
7. Tunza kumbukumbu zote zinazohusiana na mzigo wako
Mzigo unapotoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine taarifa za vituo hutumwa kwa muhusika ili kujua maendeleo ya mzigo wake. Jambo la msingi hapa ni kutunza taarifa zote zinazohusiana na mzigo ili kukurahisishia ufuatiliaji na upokeaji wa mzigo. Licha ya hivyo, utunzaji wa taarifa hutumika na mnunuzi anapotaka kusitisha oda yake au kuripoti mapungufu ya bidhaa iliyoagizwa. Kuna njia mbalimbali za kutunza taarifa za mzigo wako mojawapo ni kumbukumbu ya email ya kukubali oda ya bidhaa.