NJIA BORA YA KUCHAGUA BIDHAA MTANDAONI

Ingia katika mtandao wowote ambao unapenda kununua bidhaa mfano ebay.com, shopify.com au aliexpress.com kisha katika sehemu ya ku search andika jina la bidhaa unayohitaji kununua.
zitatokea bidhaa nyingi kutoka kwa wauzaji mbalimbali. Mara nyingi bidhaa zitakua zinatofautiana bei sasa ni kazi yako kuchagua bidhaa yenye bei nafuu. Kisha ingia katika mtandao mwingine na ulinganishe bei ya bidhaa ile ile ili upate unafuu zaidi, mfano kama ulianza na aliexpress.com sasa nenda ebay.com ili upate kulinganisha bei. Unafuu wa bei hautoshelezi kama kigezo pekee cha wewe kununua bidhaa kutoka kwa muuzaji huyo wa bei nafuu, kuna vitu vingine pia vya kuzingatia kama inavyohainisha hapa chini.

Gharama ya usafiri
Angalia njia ya usafiri muuzaji atakayotumia na gharama yake, muuzaji anaweza kukuandikia bei nafuu ya bidhaa lakini bei ya usafiri ikawa kubwa zaidi.
Nashauri mtu anayenunua bidhaa mtandaoni kuchagua njia ya usafiri inayotumia ndege ili kufanya bidhaa zako kufika mapema zaidi ukilinganisha na mzigo ukisafirishwa kwa njia ya meli. Kwa mtu anayetumia aliexpress tunashauri sana atumie njia ya aliexpress standard shipping kwani ni nafuu sana mfano kama umenunua bidhaa ya 50,000/= unaweza kulipia 3,000/= tu kama gharama ya usafiri.
Usipende kutumia DHL kwa sababu ni gharama sana, unaweza nunua bidhaa ya 5,000/= tu lakini usafiri ukakugharimu 50,000/= au na zaidi. DHL ni nzuri kama unanunua bidhaa nyingi zinazogharimu pesa nyingi.


Free shipping
Free shipping inamaanisha ukinunua mzigo hauna haja ya kulipia gharama za usafiri. Sio kweli kwamba ukitumia free shipping mzigo wako unachelewa kufika, kuchelewa kufika kwa mzigo inategemea na njia ambayo mzigo utapitia, kama ni meli au ni ndege au ni office za posta za huko unakonunua mzigo. Wauzaji wengine hutoa free shipping lakini mzigo unakufikia haraka zaidi ya hata ungelipia mzigo wako. Nikitolea mfano aliexpress.com wananjia inayoitwa aliexpress standard shipping ambayo ndio njia ya gharama nafuu na mzigo wako unafika haraka ndani ya siku 10 hadi 18 unakua umeupata. Ukikuta muuzaji katumia njia hii kwenye free shipping basi jua mzigo wako unafika haraka. Ila ukikuta muuzaji katumia njia ya small packets delivery method jua mzigo wako utatumia mwezi mzima kufika. 

Muuzaji Mwaminifu
Ununuaji wa bidhaa mtandaoni kwa sasa unaaminika sana ukilinganisha na miaka kama mitatu nyuma iliyopita. Lakini inapaswa ufahamu kwamba sio kila muuzaji wa online anaaminika, unaweza nunua kitu lakini kikafika kibovu, unaweza nunua kitu lakini kikafika sio kama maelezo yalivyotolewa kwenye product description, unaweza nunua kitu lakini kikafika kwa kuchelewa sana. hivyo basi unaponunua kitu hakikisha unasoma feedback za waliokwisha nunua bidhaa hiyo kabla hujalipia au hakikisha positive feedback iwe zaidi ya asilimia 80% kwani kila bidhaa mtandaoni inapewa feedback na watu waliokwisha nunua sio tu hivyo bali pia angalia rating ya seller iwe angalau 4.3 out of 5.0. pia angalia bidhaa hiyo ni wangapi wamenunua, kila bidhaa inaonyesha idadi ya watu ambao tayari walikwisha nunua, nunua bidhaa kwa muuzaji ambaye bidhaa yake imenunuliwa zaidi. 
Wauzaji hawa wana orders nyingi


Njia ya kulipia bidhaa
Hii pia ni muhimu japokua sio sana. katika njia za kulipia bidhaa, ukitumia card ya bank (visa au mastercard) makato yanakuwa kidogo ukilinganisha na ukitumia njia nyingine za ulipaji kwani makato (service charges) yanakua juu. Ili upate faida nzuri, chagua muuzaji mwenye njia ya ulipaji yenye makato nafuu. Ukitumia western union au bank wire gharama za makato zinakua juu zaidi.

Mawasiliano na muuzaji
Hii ni uhimu sana kwa wanunuaji wa bidhaa za jumla. Mfano mtu unahitaji kununua bidhaa 300 za aina moja mtandaoni. kabla hujafanya ku order mzigo wako, hakikikisha unafanya mazungumzo na muuzaji kwanza, ikibidi akutumie sample kabla hujanunua kitu chochote. akuambie gharama za usafiri zimekaaje ili ukipiga hesabu ujue kama faida inapatikana au lah. kumbuka kodi ni kama 44.5% ya bei ya bidhaa, hivyo muulize seller ni bei gani ataandika kwenye transaction value ili ujue kodi utakatwa asilimia ngapi. Kila mtandao unakitu kinaitwa contact seller kinakuwezesha ku chat na muuzaji kabla hujalipia bidhaa. 

Kumbuka: kwa wanunuaji wa bidhaa za jumla nashauri watumie alibaba.com kwani utanunua bidhaa zako kwa bei nafuu zaidi kutoka viwandani moja kwa moja.

Featured Post

Jifunze kununua mtandaoni

Karibu katika somo la kwanza ujifunze ni jinsi  gani unaweza kununua bidhaa kutoka mataifa makubwa duniani kwa kutumia mitandao mikubwa ka...