BEI NAFUU
Bidhaa nyingi zinazouzwa mtandaoni zina punguzo kubwa la bei, hii ni kutokana na ukweli kwamba wauzaji wa bidhaa ndio wamiliki.
Bidhaa nyingi tunazonunua madukani zinapitia mikononi mwa wauzaji wengi (middle man) ambapo kila muuzaji huongeza kiasi cha bei ili apate faida. Fikiria namna hii, bidhaa inatoka China kwa mzalishaji mkubwa, inapita kwa watu wafuatao kabla ya kukufikia, wamiliki wa makontena bandarini, wauzaji wa jumla kuu, wauzaji wa jumla ya kati, wauzaji wa jumla ndogo, wasafirishaji wa mizigo/vifurushi na wauzaji wa rejareja. Mtiririko uliooneshwa hapo juu unafanya gharama ya bidhaa kuwa kubwa sana. Licha ya hivyo gharama za kodi huongezeka mno kiasi ambacho gharama ya bidhaa hufikia hadi mara tatu ya gharama halisi kabla haijauzwa kwa mtumiaji. Kuepuka gharama hizi kubwa ni vema kuagiza bidhaa yako mtandaoni na kuokoa fedha zako.
Unapotembelea maduka mengi na kununua bidhaa ambayo haina ubora huwa inakua changamoto sana kurudishiwa fedha yako. Hii ni kutokana na ukweli kwamba muuzaji wa duka ndio mmiliki wa ile bidhaa, lakini kwa wauzaji wa mtandaoni mmiliki wa bidhaa, mwenye mtandao na mnunuzi ni watu watatu tofauti. Wauzaji wengi wa mtandaoni huwa hawatumi fedha moja kwa moja kwa uzaji wa bidhaa mpaka bidhaa ikufikie na uridhike nayo. Endapo bidhaa uliyoipata itakuwa na mapungufu wamiliki wa e-commerce hurudisha fedha za mnunuzi kwenye account yake kwa kutumia mifumo husika. Hili ni jambo zuri sana, jambo la kuzingatia kwako wewe kama mnunuaji ni kuhakikisha bidhaa unayonunua imeunganishwa na mifumo hio.
Bidhaa nyingi zinazouzwa mtandaoni zina punguzo kubwa la bei, hii ni kutokana na ukweli kwamba wauzaji wa bidhaa ndio wamiliki.

UFANISI WA MANUNUZI
Mara kwa mara wanunuzi wengi wamekuwa wakipita katika maduka makubwa ( Super markets/ Stores) majira ya jioni lakini changamoto inakuja pale unapokosa bidhaa unayoitaka, katika hali kama hii mnunuzi anakuwa amepoteza muda wake na fedha zake, kwa kulitambua hili wauzaji wa mtandaoni (e-Commerce) wamerahisi upatikanaji wa bidhaa nyingi mahali pamoja. Ni rahisi kwa mnunuzi kuingia mtandaoni muda wowote na kutafuta bidhaa. Hii inaokoa muda sana, hususani kwa wanunuzi wenye majukumu mengi. Na endapo mnunuzi atakosa bidhaa anayoitafuta atakuwa na uhuru mkubwa wa kuingia katika mtandao mwingine na kuchagua bidhaa anayoitaka.
UHAKIKA WA FEDHA

HAKUNA MSONGAMANO
Kwa wanunuzi wengi wa masoko na maeneo mbalimbali changamoto inayowafanya watu wengi wasiende maeneo kama Kariakoo ni msongamano wa watu unaombatana na changamoto za usafiri pamoja na matukio yasiyo ya kiusalama katika maeneo hayo. Kuepuka usumbufu huo wote baadhi ya watu huamua kununua bidhaa mtandaoni na kuokoa muda wao mbali na usumbufu wa aina hizo. Fikiria namna hii, unapoamua kutoka na kwenda kufanya shopping, gharama ya usafiri, msongamano wa magari barabarani, matrafiki, wezi wa kariakoo na joto la kutosha. Ukweli ni kwamba kwa mtu anayethamini muda wake ataepuka usumbufu huo wote kwa kununua/agiza vitu mtandaoni.
URAHISI WA KUPATA BIDHAA ZILIZOTUMIKA (USED)
Ni maeneo machache unaweza kupata bidhaa iliyotumika na ukaridhika nayo, licha ya hivyo baadhi ya wauzaji wa mtandaoni wamelirahisisha hili kwa kuruhusu wauzaji kuuza bidhaa zilizotumika mtandaoni. Unachotakiwa kukifanya ni kuwasiliana na muuzaji na kupata taarifa sahihi za kitu unachotaka kukinunua. Mtandao wa kupatana.com ni mojawapo mitandao inayomuunganisha muuzaji na mnunuzi pasipo gharama yoyote. Linabaki kuwa jukumu lako wewe kama mnunuzi kufuatilia ni bidhaa inayonifaa, ili kutatua changamoto niliyo nayo.
ULINGANIFU WA BEI
Kati ya changamoto ambazo wanunuaji wanakutana nazo ni kujua, Je hii ni bei sahihi? Ni vigumu kwa mnunuzi kulinganisha bei ya bidhaa kutoka duka moja hadi duka lingine. Lakini kwa wanunuaji wa mtandaoni ni rahisi sana kulinganisha bei toka muuzaji mmoja hadi muuzaji mwingine, hii husaidia sana kupunguza hasara ambayo mnunuzi angeipata kama ungeamua kutembea toka duka moja hadi duka lingine. Si hivyo tu mnunuzi anapata nafasi ya kulinganisha bei hizo pasipo kushawishiwa na maneno ya muuzaji, anachotakiwa kuwa nacho mnunuzi ni upatikanaji wa intanet ya uhakika na kompyuta/smartphone.
USIRI WA MANUNUZI
Licha ya faida zote tajwa hapo juu kuna jambo lingine la msingi sana kwa mnunuaji, nalo ni usiri wa manunuzi. Ni ukweli usiofichika kuna baadhi ya vitu ambavyo wanunuzi huwa hawapendi kuonekana wakivinunua hadharani au kukutana na wauzaji wa bidhaa. Kuna baadhi ya wanaume huona aibu kununua nguo za kike, kuna baadhi ya wanawake huona aibu kununua nguo za kiume, kuna baadhi ya vitu huwa ni changamoto kuuzwa hadharani mfano. Mipira ya kinga (Condoms). Ni mazingira ya e-commerce pekee, yanayotoa uhuru wa namna hii.