Karibu katika somo la kwanza ujifunze ni jinsi gani unaweza kununua bidhaa kutoka mataifa makubwa duniani kwa kutumia mitandao mikubwa kama vile Aliexpress.com, alibaba.com, amazon.com ,shopify.com, ebay.com
Katika mitandao hii utajipatia bidhaa za kipekee ambazo sio rahisi kuzipata huku Tanzania.

Sio hivyo tu pia unajipatia bidhaa mbalimbali kwa bei nafuu sana ambapo pengine huku Tanzania utauziwa bidhaa hiyohiyo hata mara tatu ya bei ambayo utanunua mtandaoni.
Somo hili la kwanza ni kukuhakikishia kuwa mitandao hii ni ya uhakika na huwezi kupoteza pesa zako unaponunua bidhaa mtandaoni kwa kufuata maelekezo sahihi ambayo yatatolewa katika mfululizo wa masomo yetu.
Kitu cha kwanza kufahamu kuhusu mitandao hii, ni muhimu sana kujua mitandao ipi ni bora kwa makundi gani. Makundi ninayoongelea hapa ni kwa wanunuaji kati ya wanunuaji wa rejareja na wale wanunuaji wa vitu vya jumla.
Aliexpress.com, amazon.com ,shopify.com, ebay.com ni mitandao bora kwa wanunuaji wa rejareja au wafanyabiashara wadogo wadogo ambao hawahitaji kununua bidhaa nyingi sana kwa pamoja mfano bidhaa zisizozidi 200.
Alibaba.com ni mitandao ambayo inafaa sana kwa wanunuaji wa jumla mfano kuanzia bidhaa 200 za aina moja hususani kwa wale wanaotaka kuagiza moja kwa moja kutoka viwandani, kwa mawakala, kwa watengenezaji na wasafirishaji (exporters).

Kitu cha pili ambacho inapaswa ufahamu kuhusu hii mitandao ni kwamba mzigo wako usipokufikia unarudishiwa pesa yako. Hivyo basi kaa ukifahamu na ukiamini kuwa mitandao hii ni ya uhakika kabisa.
Mitandao hii ina mifumo madhubuti inayomlinda mnunuaji pale anapofanya manunuzi mtandaoni ili kumlinda dhidi ya wauzaji wasio waaminifu na kukuwezesha kurudishiwa fedha zako kama bidhaa isipokufikia, Alibaba.com wana mfumo wa trade assurance, Aliexpress.com wanatumia mfumo wa Buyer protection na ebay.com wanatumia mfumo wa money back guarantee .
Mifumo hii inamlinda mnunuaji wa bidhaa kwa kumrudishia fedha zake, pale ambapo muuzaji wa bidhaa anaposhindwa kufikisha bidhaa ndani ya muda uliopangwa au kuleta bidhaa isiyo na ubora stahiki.

Mifumo hii itakupa nafasi ya kutoa taarifa ndani ya muda wa siku 15 baada ya siku 60 za kukamilisha oda, zikipita siku hizo hujatoa taarifa yoyote ile kuhusu kitu ulichoagiza hautorudishiwa pesa yako. Unaruhusiwa kutoa malalamiko baada ya siku 45 tokea umelipia mzigo wako. Unapokuwa unafanya manunuzi mtandaoni ni jukumu lako kama mnunuaji kuangalia kama bidhaa unayoagiza imejumuishwa kwenye mifumo hii ili kupunguza uwezekano wa wewe kuingia hasara na kupoteza fedha zako pale bidhaa isipofika.
Ukweli ni kwamba bidhaa zinazoagizwa mtandaoni huwa na unafuu mkubwa wa bei na endapo mnunuaji atapata elimu sahihi itakuwa ni rahisa kwake kupata bidhaa bora anazozihitaji. Maelekezo mengine tutakayokuwa tukipeana katika mafunzo haya yatakusaidia kuongeza ufanisi wako katika miamala yako inayofanyika mtandaoni.